
Company Name
Company Website
Company Email
Address
sector
Location
Company Description
Imeazishwa rasmi February 2022 ili kusaidia na kutoa fursa kwa wabunifu na wawekezaji mbali mbali, pamoja na mambo mengine, shughuli za kutoa ushauri na usimamizi wa miradi mbali mbali inayofanyiwa uwekezaji na wanachama wake.
HUDUMA ZA KAMPUNI
1. Uwekezaji; hapa tuna uwekezaji wa aina mbili, ambazo ni;
a) Uwekezaji binafsi; uwekezaji huu unafanywa na kampuni binafsi kwenye bunifu bora za biashara, zabuni au miradi kutoka kwa wanachama wetu wabunifu au kampuni zingine bila kushirikisha wanachama wetu wawekezaji.
b) Uwekezaji shirikishi; uwekezaji huu unafanywa na wanachama wetu wawekezaji baada ya sisi kutafuta bunifu bora za biashara, zabuni au mirida bora ya kufanya uwekezaji kutoka kwa wanachama wetu wabunifu na kuwashirikisha wao kufanya uwekezaji. Huku sisi tukiwa wasimamizi wakuu wa uwekezaji huo ili kuzuia hatari za kupata hasara na kuhakikisha mradi unakuwa na kutoa faida stahiki na zaidi.
NYOGEZA HAPA.
Pia tuna aina mbili za Miradi ya uwekezaji, ambayo ni;
• Miradi ya muda mfupi; mfano uwekezaji wa kwenye zabuni au mradi wowote wenye kikomo cha muda.
• Miradi ya muda mrefu; mfano ufunguzi wa biashara mpya ambayo haina kikimo cha muda.
2. Ubunifu; hapa tunatoa njia stahiki za utatuzi wa matatizo kwa wateja wetu zinazoendana na wakati, gharama na urahisishaji wa kazi ili kuongeza mapato na ufanisi kwenye biashara zao, pia tunasaidia jamii, nchi na dunia kiujumla kutatua changamoto mbali mbali. Tunakamilisha hili sisi binafsi na kwa kushirikiana na wanachama wetu wabunifu.
3. Ushauri; hapa tunatoa ushauri kiujumla; ushauri wa biashara, uwekezaji na ubunifu. Mfano biashara gani ufanye? uwe na timu ya namna gani? na nini ufanye ili kukuza biashara yako? unaweze kuwekeza wapi kutokana na malengo yako ya maisha? Manufaa ya uwekezaji na hatari zake! Pia kwa namna gani unaweza kupata ubunifu au kuwa mbunifu? Na namna ubunifu wenye manufaa utakavyobadilisha maisha yako n.k.
MISHENI YA KAMPUNI
Kuwasaidia wanachama wetu kufikia malengo yao ya kifedha huku tukiwa na matokeo chanya katika jamii kupitia uvumbuzi, uwekezaji na ushauri.
MAONO YA KAMPUNI
Ili kutoa maisha bora, fursa, uhuru wa kifedha kwa wanachama wetu, wanahisa, washirika na kukua kama kampuni inayoongoza duniani ya uwekezaji.
MALENGO YA KUINGIA KWENYE PROGRAMU YA ENDELEZA.
Lengo ni kujifunza namna bora zaidi za kuijenga biashara ili kuweza kujijengea uwezo wetu binafsi na kuvutia wadau mbali mbali kufanya kazi nasi, kutokana na huduma tunazotoa.